Isaiah 32:9-13

Wanawake Wa Yerusalemu


9 aEnyi wanawake wenye kuridhika sana,
amkeni na mnisikilize.
Enyi binti mnaojisikia kuwa salama,
sikieni lile ninalotaka kuwaambia!

10 bMuda zaidi kidogo ya mwaka mmoja,
ninyi mnaojisikia salama mtatetemeka,
mavuno ya zabibu yatakoma
na mavuno ya matunda hayatakuwepo.

11 cTetemekeni, enyi wanawake wenye kuridhika,
tetemekeni kwa hofu, enyi binti mnaojisikia salama!
Vueni nguo zenu,
vaeni nguo ya gunia viunoni mwenu.

12 dPigeni matiti yenu kwa ajili ya mashamba mazuri,
kwa ajili ya mizabibu iliyozaa vizuri

13 ena kwa ajili ya nchi ya watu wangu,
nchi ambayo miiba na michongoma imemea:
naam, ombolezeni kwa ajili ya nyumba zote za furaha
na kwa ajili ya mji huu wenye kufanya sherehe.
Copyright information for SwhKC